PAKA

Paka wewe paka gani, Sielewi unadhiki Paka kutwa nakulani, Hutoki huwajibiki Paka kakufunza nani?, Uzembe uloshiriki Paka toka kwangu ndani, Kuwa nawe siridhiki Paka mithili ya nyani, Pata-shika hushikiki Paka we huna thamani, Tabia hazisifiki Paka hutoki uwani, Majungu hayadiriki Paka toka kwangu ndani, Kuwa nawe siridhiki Paka si wa jalalani, Panya kwako si riziki … Continue reading PAKA

NYOYO ZETU

Kwa moyo mie nakiri, Natamka kwa ulimi Nyota nimeitabiri, Nikawa sina usemi Bora nifichue siri, Ninayempenda mimi Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Macho hayakukosea, Yalipokuona wewe Na nafsi kungojea, Nikangiwa na kiwewe Huu wangu upokea, Moyo nakupa mwenyewe Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Zama za tokea enzi, Nilikupenda kwa dhati Moyo … Continue reading NYOYO ZETU