CHURA NAMBA 20!

sehemu ya 1 1.Eneo la Kiwalani, Saa kumi za jioni, Meweka gari pembeni, Kumngoja abiria. 2.Kapungia kwa yakini, Na mimi sikumuhini, Karibu na kituoni, Breki nikakanyagia. 3.Akafika dirishani, Anitazama usoni, Na mtoto mgongoni, Ngata amemfungia. 4.Ndipo nikashuka chini, Nikazunguka pembeni, Nikaenda mlangoni, Ili kumfungulia. 5.”Chura namba ishirini, Karibu na Mkunguni, Ni mtaa wa mjini, Pesa … Continue reading CHURA NAMBA 20!

Rabi Nipa Subira

Rabi Nipa Subira Mengi mnanizushia, kiasi nione dhiki, Ubaya mnanitia, pamwe na kunihiliki, Ya Rabi navumilia, japo hayavumiliki. Mwaenda kila mahali, sihiri kuishiriki, Mnafanya kulahali, kuziba yangu riziki, Ya Rabi nayakubali, japo hayakubaliki, Mmenivisha na nira, ilo nzito mahuluki, Na sasa sinayo dira, mbee hakupambauki, Ya Rabi nipa subira, japo hayasubiriki. Continue reading Rabi Nipa Subira

SITAKI TENA!

Usambe sitendi haki, kwa haya kukuambia, Sitaki tena sitaki, japo kunikaribia, Sivyo nitakushitaki, na jela nitakutia. Hata ukinipa laki, ya Dola ama Rupia, Sibaki tena sibaki, sasa nafuata njia, Kama riziki Razaki, peke atanipatia. Si neno wabaramaki, kwa dogo unachukia, Shitaki tena shitaki, kwa ndugu jamaa pia, Ila pano sitabaki, niate nifate ndia. Tama sitataharaki, … Continue reading SITAKI TENA!

JUMATATU

Jina langu jumatatu, Mkongwe wa familia Nisiyependwa na watu, Siku yangu kiwadia Damu yangu ina kutu, Ndugu zangu wanambia Wanadamu mna hila, Mbona mwanipakazia? Jumatatu nikifika, Nyote mnakunja sura Hakuna anoridhika, Kama haja ya dharura Waja mnakasirika, Na mijuso ikafura Wanadamu mna hila, Mbona mwanipakazia? Japo nafungua wiki, Hakuna anosifia Eti siku ina dhiki, Mwazidi … Continue reading JUMATATU

DEBE TUPU

Mja lojaliwa domo, Na uzuri wa lisani Wasema pasi kikomo, Maneno yasothamani Kulaghai pia umo, Waja wawadanganyani? Ama kweli debe tupu, Haliwachi kuitika Upunguze chokochoko, Kuchochea majirani Sizuwe na sokomoko, Ukasutwa hadharani Wakubatize ‘mnoko’, Jina likabwaga zani Ama kweli debe tupu, Haliwachi kuitika Kama huna la kusema, Jifunge zipu kinywani Uwache wenye hekima, Kauli hamulingani … Continue reading DEBE TUPU

NATAFUTA MSICHANA

NATAFUTA MSICHANA Ewe Mola nijalie, Mtukufu Maulana Naomba nitunukie, Nimpate huyu mwana Ombi langu lisikie, Nipate kuitwa bwana Natafuta msichana, Mwenyezi niitikie Moyoni nihifadhie, Asinikane hapana Kwake niwe mpenzie, Anipende kiungwana Kukicha awe na mie, Penzi letu litafana Natafuta msichana, Mwenyezi niitikie Tungo mi nimtungie, Ili anipende sana Shairi nimwandikie, Nikaririe bayana Na tenzi nimuimbie, … Continue reading NATAFUTA MSICHANA

MKE BORA

Nipani mke wa haya, Aepukaye maudhi Hadithi nyingi na aya, Moyoni alohifadhi Buibui la ‘habaya’, Vazi lake lenye hadhi Mke alo na kasoro, Kuoa ni mke bora Nipani mke kipofu, Huku kule hatazami Mbonize sio potofu, Aonacho halalami Kuwa naye hana hofu, Haulizi hasimami Mke alo na kasoro, Kuoa ni mke bora Nipani mke kiziwi, … Continue reading MKE BORA

KWETU SIJE KUKAOZA

KWETU SIJE KUKAOZA Kina kaka na madada, Wanafunzi mahodari Mliotuzwa shahada, Mkatanua vidari Nimewaletea mada, Iwafikie habari Tufanyeni hala hala, Kwetu sije kukaoza Mumeshapiga hatua, Mukaivuka mipaka Na ulaya mkatua, Taaluma kuisaka Mtokako mwatambua, Wasubiri bila shaka Tufanyeni hala hala, Kwetu sije kukaoza Matatizo yamezidi, Hilo kwanza mkubali Kutatua inabidi, Zimeedhoofika hali Lazima mjitahidi, Msiseme … Continue reading KWETU SIJE KUKAOZA

VIUMBE WAZITO

 VIUMBE WAZITO Waja viumbe wazito, Mwenyezi alowaumba Nawasuta kwa misuto, Kinyoshea dole gumba Situtie tumbo joto, Kututishia kwa ndumba Akuvikaye ugumba, Huwa keshaitwa tasa Kila njama za mikato, Masahibu kutukumba Badala ya manukato, Mwatumwagilia vumba Maneno maji ya moto, Hayateketezi nyumba Akuvikaye ugumba, Huwa keshaitwa tasa Kututengea kushoto, Kwa mizaha mkitamba Kila jambo liwe zito, … Continue reading VIUMBE WAZITO

TENDE NA HALUWA

Naamba na waswahili, Magwiji wataalamu Wanijibu swali hili, Wa’mbe nipate fahamu Wafafanue kamili, Kung’amua ng’amu ng’amu Penye tende na haluwa, Kipewa nitwae gani? Sitaki kutwaa mbili, Moyo moja unahamu Kuchanganya mie sili, Kuuvuruga utamu Nasifu zote jamili, Ulaji wa nyamu nyamu Penye tende na haluwa, Kipewa nitwae gani? Haluwa bei ni ghali, Huliwa kwenye karamu … Continue reading TENDE NA HALUWA